Rais Xi Jinping apongeza miaka 70 ya Shirikisho Kuu la Viwanda na Biashara la China (ACFIC)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2023
Rais Xi Jinping apongeza miaka 70 ya Shirikisho Kuu la Viwanda na Biashara la China (ACFIC)
Wang Huning, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma wa China (CPPCC) akihudhuria mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Viwanda na Biashara la China (ACFIC) na kutoa hotuba mjini Beijing, China, Oktoba 24, 2023. (Xinhua/Yan Yan)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza kuhamasisha watu binafsi katika sekta ya kibinafsi ya China kushikamana kwa karibu zaidi na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na kutafuta maendeleo makubwa mapya katika kazi ya mashirikisho ya viwanda na biashara.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo katika barua ya pongezi kwa Shirikisho Kuu la Viwanda na Biashara la China (ACFIC) kwa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake.

Kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, Rais Xi ametoa salamu kwa maafisa na wafanyakazi wa ngazi zote za mashirikisho ya viwanda na biashara na watu binafsi katika sekta ya kibinafsi kote nchini China.

Akipongeza kazi yao katika miaka 70 iliyopita, Rais Xi amesema mashirikisho ya viwanda na biashara yametoa mchango muhimu kwa maendeleo ya Jamhuri ya Watu wa China, kuendeleza mageuzi na ufunguaji mlango, na kujitoa kwa juhudi kubwa katika kujenga zama mpya.

Katika barua hiyo, Rais Xi amehimiza juhudi za kuwezesha maendeleo yenye sifa bora ya sekta isiyo ya umma na wale wanaofanya kazi ndani yake, na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu ya sekta ya kibinafsi.

Rais Xi ametoa wito kwa watu binafsi katika sekta ya kibinafsi kutumia kikamilifu falsafa mpya ya maendeleo na kushamirisha ujasiriamali, kuchangia katika kujenga nchi ya kijamaa ya kisasa katika mambo yote na kuendeleza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China katika nyanja zote.

Mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa ACFIC umefanyika Beijing siku ya Jumanne. Wang Huning, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma wa China (CPPCC) alihudhuria hafla hiyo na kutoa hotuba.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha