Nchi wanachama wa BRICS zakubali kuzidisha ushirikiano ili kuhimiza uimarikaji endelevu wa utalii

(CRI Online) Oktoba 25, 2023

Nchi wanachama wa BRICS ambazo ni pamoja na Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zimekubaliana kuzidisha ushirikiano ili kufikia uimarikaji endelevu na jumuishi kwenye sekta ya utalii.

Nchi hizo zimeeleza hayo katika taarifa ya pamoja iliyosainiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa utalii wa nchi za BRICS iliyotolewa siku ya Jumanne mjini Cape Town. Mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Uimarikaji endelevu na jumuishi kwenye sekta ya utalii” utaendelea kwa siku tatu hadi tarehe 26 Oktoba.

Taarifa hiyo inasema nchi wanachama wa BRICS zinatambua athari kubwa zilizotokana na janga la COVID-19 kwenye sekta ya utalii, lakini janga hilo pia limeleta fursa ya kutekeleza mageuzi wakati sekta ya utalii inatengeneza mustakabali imara na jumuishi zaidi.

Imesema, ili kufikia uimarikaji endelevu na ulio rafiki kwa mazingira wa sekta ya utalii kunahitaji kuanzisha na kufuata zaidi sera imara na endelevu za mazingira na utamaduni wa kijamii.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha