China yaahidi kuhimiza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2023
China yaahidi kuhimiza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Tanzania
Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian (wa pili kulia) akitoa taarifa ya matokeo ya Mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja uliofanyika Beijing, China wiki iliyopita wakati wa mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 26, 2023. (Xinhua/ Li Yahui)

DAR ES SALAAM - Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, amesema China inatarajia kuendelea kuhimiza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Tanzania, ili kwa pamoja kuendeleza mustakabali mzuri wa baadaye wa maendeleo ya kisasa.

Balozi Chen ameyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam, Tanzania, ambapo aliwasilisha taarifa ya matokeo ya Mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja uliofanyika Beijing, China uliofanyika Beijing, China wiki iliyopita.

Ameangazia maendeleo yaliyopatikana katika ushirikiano wa nchi hizo mbili kwenye Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) katika muongo mmoja uliopita, hasa katika maendeleo ya miundombinu, uchumi na biashara, uwekezaji na mabadilishano kati ya watu.

Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kutumia uwezo wa kifursa kuimarisha muunganisho wa miundombinu, kuboresha mabadilishano ya kibiashara na kiuchumi na kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika maendeleo ya kijani, uchumi wa kidijitali na uchumi wa bluu.

Zaidi ya hayo, Balozi Chen amebainisha kuwa mkutano huo ulivutia wawakilishi zaidi ya 10,000 kutoka nchi 151 na mashirika 41 ya kimataifa, na kuuelezea kama tukio la kihistoria.

Baraza hilo limeadhimisha miaka 10 tangu kuanza kwa BRI, ambapo China imesaini mikataba zaidi ya 200 ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na nchi zaidi ya 150 na mashirika 30 ya kimataifa.

Balozi Chen amesema mwaka 2024 utakuwa ni mwaka maadhimisho ya miaka 60 tangu China na Tanzania zianzishe uhusiano wa kidiplomasia, akisema China iko tayari kutumia Baraza hilo kama fursa ya kushirikiana na washirika wa Tanzania katika kutatua changamoto na kutafuta maendeleo ya pande zote mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha