

Lugha Nyingine
Wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-16 wako tayari kurejea duniani baada ya makabidhiano ya waananga wa Shenzhou-17 walioko kwenye obiti
Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Safari ya Anga ya Juu cha Beijing, Oktoba 26, 2023 ikionyesha Wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-16 na Shenzhou-17 wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kituo cha anga ya juu cha China. (Picha na Han Qiyang/Xinhua)
JIUQUAN - Wanaanga wa China wa Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-16 wamekabidhi udhibiti wa kituo cha anga za juu cha China, Tiangong kwa wanaanga wapya wa chombo cha Shenzhou-17 waliowasili Jumapili, limesema Shirika la Anga ya Juu la China.
Wanaanga hao wa vyombo hivyo viwili wamefanya hafla ya makabidhiano baada ya wanaanga wa chombo hicho cha Shenzhou-16 kumaliza kazi zote zilizopangwa. Wanatarajiwa kurejea duniani Oktoba 31 wakiwa kwenye chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-16.
Eneo la Kutua la Dongfeng, lililoko katika Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China, linajiandaa kwa ajili ya kurejea kwa chombo cha Shenzhou-16 kutoka anga ya juu.
Hii itakuwa safari ya tano ambapo eneo hilo la kutua limefanya kazi ya utafutaji wa sehemu za chombo cha anga ya juu na kupokea wanaanga.
Wafanyakazi wa ardhini wamepitia mazoezi mbalimbali ya utafutaji na uokoaji kwa ajili ya safari hiyo ijayo, mamlaka za eneo hilo la kutua zimesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma