Israel yaongeza mashambulizi ya ardhini katika Ukanda wa Gaza

(CRI Online) Oktoba 30, 2023

Israel imeongeza mashambulizi ya ardhini katika Ukanda wa Gaza na kuongeza mashambulizi ya anga katika eneo hilo lililozingirwa huku idadi ya watu waliouawa katika Ukanda wa Gaza wa Palestina ikifikia 8,005.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel Daniel Hagari amesema, jeshi hilo limeongeza askari wake wanaoingia kwenye Ukanda wa Gaza, huku akiongeza kuwa, operesheni za sasa za ardhini zinalenga zaidi sehemu ya kaskazini ya Ukanda wa Gaza.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant Jumapili alikutana na wawakilishi wa familia za watu 230 waliotekwa nyara na kundi la Hamas katika mashambulizi ya tarehe 7 mwezi huu dhidi ya Israel, na kusema kuwa, mashambulizi ya ardhini ni sehemu ya juhudi za kuwaokoa mateka hao.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha