Rais Xi Jinping asisitiza kuandaa, kuwahamasisha wanawake kuchangia katika maendeleo ya kisasa ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 31, 2023

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu wakati wa mazungumzo na maofisa viongozi wapya wa Shirikisho Kuu la Wanawake wa China mjini Beijing, China, Oktoba 30, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu wakati wa mazungumzo na maofisa viongozi wapya wa Shirikisho Kuu la Wanawake wa China mjini Beijing, China, Oktoba 30, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

BEIJING- Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) siku ya Jumatatu kwenye mazungumzo na maofisa viongozi wapya wa Shirikisho Kuu la Wanawake wa China (ACWF) ametoa wito wa juhudi za kuhamasisha na kushirikisha wanawake kuchangia nguvu zao kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China na kusisitiza kufuata njia ya ujamaa wenye umaalum wa China kwa maendeleo ya wanawake.

Rais Xi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesisitiza kuwa, katika kujenga mambo ya kisasa ya China kwa kuhimiza ujenzi wa nchi wa pande zote ili China iwe nchi yenye nguvu kubwa na kufikia ustawishaji mkubwa wa Taifa la China inahitaji watu wote wa China kushikamana na kufanya kazi pamoja, ambapo mchango wa wanawake hauna mbadala.

Amesema, tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC Mwaka 2012, Kamati Kuu ya Chama imeimarisha uongozi wake kwa ujumla kuhusu mambo ya maendeleo ya wanawake, kuimarisha mfumo wa sheria wa kulinda haki na maslahi ya wanawake, na kuboresha mazingira kwa ajili ya maendeleo ya wanawake.

Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mashirikisho ya wanawake ya ngazi zote nchini China yametekeleza kwa dhati wajibu wao wa kuongoza, kuwahudumia na kudumisha uhusiano na wanawake.

"Yamefanya kazi nzuri katika kulinda haki za wanawake na kuwajali, na yamefanya jitihada za kuendelea kuimarisha mageuzi ya mashirikisho ya wanawake," Rais Xi ameongeza.

Ni muhimu kuimarisha miongozo juu ya mitazamo ya vijana kuhusu ndoa, uzazi na familia, amesema Rais Xi, huku akihimiza mashirikisho ya wanawake kurekebisha na kutekeleza sera za uungaji mkono wa uzazi, kuongeza ubora wa maendeleo ya idadi ya watu, na kukabiliana kwa hamasa na hali ya kuongezeka kwa idadi ya wazee katika idadi ya jumla ya watu.

Huku akieleza kuwa kulinda haki na maslahi halali ya wanawake na watoto, kuhimiza usawa wa kijinsia na maendeleo ya pande zote ya wanawake na watoto ni sehemu muhimu za maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, Rais Xi ametoa wito kwa mashirikisho ya wanawake ya ngazi zote kuongeza juhudi za kutatua matatizo makubwa ambayo huathiri na kukiuka haki na maslahi ya wanawake na watoto.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha