Wanahabari wa Eurasia washangilia mchezo wa mpira wa kikapu kijijini pamoja na maelfu ya watazamaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 31, 2023

Usiku wa tarehe 28, Oktoba, fainali ya Ligi ya Mpira wa Kikapu vijijini ya China Mwaka 2023 ilifanyika kwenye Kijiji cha Taipan kilichoko Wilaya ya Taijiang katika Mkoa wa Guizhou, China, ambapo ujumbe wa wanahabari wa vyombo vya habari vya nchi za Eurasia wanaoshiriki programu ya “Kuitazama Guizhou” walikaa jukwaani kutazama fainali hiyo wakishangilia na kupiga shangwe za nderemo pamoja na makumi ya maelfu ya watazamaji wengine.

Picha ikionesha fainali ya ligi ya mchezo wa mpira wa kikapu ya vijijini ya China Mwaka 2023. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Picha ikionesha fainali ya ligi ya mchezo wa mpira wa kikapu ya vijijini ya China Mwaka 2023. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Katika fainali hiyo, Timu ya Shaxi na Dalong kutoka Mkoa wa Guangdong wa China zilishindana vikali.

Ujumbe wa wanahabari wa vyombo vya habari vya nchi za Eurasia wanaoshiriki programu ya “Kuitazama Guizhou” wakiwa jukwaani kutazama michezo. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Ujumbe wa wanahabari wa vyombo vya habari vya nchi za Eurasia wanaoshiriki programu ya “Kuitazama Guizhou” wakiwa jukwaani kutazama michezo. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

“Hamasa ya uwanjani ni kubwa sana! Kabla ya kuja hapa, sikujua mchezo wa mpira wa kikapu kijijini unaweza kuvutia ufuatiliaji wa umati mkubwa namna hiyo. Wakati nikitazama mchezo, nilibaini kwamba, kulikuwa na wanaume na wanawake, na wazee na watoto, wakiwemo watoto wa miaka mitatu au minne wakitazama mchezo moja kwa moja uwanjani. Hali ya uwanjani ilikuwa yenye shamrashamra, hata nilitaka kupiga kelele pamoja na watazamaji wengine” amesema Umatkul Bralkieva, meneja wa mambo ya kibiashara wa gazeti la Slovo Kyrgyzstana kutoka Kyrgyzstan baada ya kutazama mchezo huo.

Picha ikionesha viti vyote vikiwa vimekaliwa na watazamaji kwenye fainali ya mchezo wa Ligi ya mpira wa kikapu ya vijijini. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Picha ikionesha viti vyote vikiwa vimekaliwa na watazamaji kwenye fainali ya mchezo wa Ligi ya mpira wa kikapu ya vijijini. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Yaraslau Danilenka kutoka Belarus amesema, idadi ya watazamaji na hali yenye shamrashamra uwanjani imemshangaza. “Watazamaji hapa siyo tu wanashangilia timu yao, bali pia wanashangilia timu pinzani.”

Mwandishi wa habari akiwa ameshika bango kwa ajili ya kuwashangilia wachezaji. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Mwandishi wa habari akiwa ameshika bango kwa ajili ya kuwashangilia wachezaji. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Inafahamika kuwa historia ya mchezo wa Ligi ya mpira wa kikapu katika Kijiji cha Taipan ilianzia mwaka 1936. Kila ifikapo “Siku ya sita, Mwezi wa sita” kwa kalenda ya jadi ya China, au Sikukuu ya kula mazao mapya, wanakijiji huko hufanya michezo ya mpira wa kikapu. Tangu michezo ya Ligi ya mpira wa kikapu ya vijijini ya China ilipoanza mwaka huu, michezo hiyo imevutia watu nchini kote China, na mchanganyiko wa michezo ya vijijini na utamaduni wa jadi wa kikabila umevutia ufuatiliaji mkubwa wa watu katika jamii.

Mwandishi wa habari wa ujumbe akishangilia uwanjani. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Mwandishi wa habari wa ujumbe akishangilia uwanjani. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha