Maafisa na askari wote wa Kikosi cha 13 cha kulinda amani cha China huko Sudan Kusini (Wau) wapewa "Nishani ya Heshima ya Amani" ya UN

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 31, 2023

Kweku Dankwa Hagan, Kamanda wa Kisekta wa Kamandi ya Magharibi ya Kikosi cha Kulinda Amani cha UN nchini Sudan Kusini akikagua gwaride pamoja na Li Hui, kamanda wa kikosi cha kulinda amani cha uhandisi cha China na kutoa nishani kwenye hafla hiyo, Oktoba 28.(Picha na Li Feiyu/Xinhua)

Tume ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kulinda amani nchini Sudan Kusini Jumamosi, Oktoba 28 ilifanya hafla ya kutoa nishani kwenye Kambi ya kikosi cha uhandisi cha China katika Kambi Kuu ya Sudan Kusini (Wau) na kutoa“Nishani ya Heshima ya Amani” ya UN kwa maofisa na askari 331 wa Kikosi cha 13 cha kulinda amani cha uhandisi na matibabu cha China (Wau) huko Sudan Kusini ili kutambua mafanikio yao mazuri waliyopata wakati wa kutekeleza operesheni ya kulinda amani na mchango wao bora katika kudumisha amani nchini Sudan Kusini.

Kweku Dankwa Hagan, Kamanda wa Kisekta wa Kamandi ya Magharibi ya Kikosi cha Kulinda Amani cha UN nchini Sudan Kusini  akiwavalisha “Nishani ya Heshima ya Amani” ya Umoja wa Mataifa askari wa kulinda amani wa China kwenye hafla hiyo. (Picha na Li Feiyu/Xinhua)

Kweku Dankwa Hagan, Kamanda wa Kisekta wa Kamandi ya Magharibi ya Kikosi cha Kulinda Amani cha UN nchini Sudan Kusini alikagua gwaride pamoja na Li Hui, kamanda wa kikosi cha kulinda amani cha uhandisi cha China.

Katika hafla hiyo Hagan alisema kuwa kikosi hicho cha China kimekamilisha kazi mbalimbali kwa kiwango cha juu, na kuchangia nguvu ya China katika kuendeleza mchakato wa amani nchini Sudan Kusini, kuonyesha wajibu wa nchi kubwa, na ni mfano wa kuigwa katika eneo hilo la kulinda amani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha