Maonyesho ya "Living Earth Expo" ya Namibia yahamasisha ulinzi na uendelevu wa mazingira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 31, 2023

Wanafunzi kutoka Shule ya Waldorf iliyoko Windhoek wakionyesha bidhaa zao za mbao kwenye Maonyesho ya Living Earth Expo  huko Windhoek, Namibia, Oktoba 28, 2023. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

Wanafunzi kutoka Shule ya Waldorf iliyoko Windhoek wakionyesha bidhaa zao za mbao kwenye Maonyesho ya Living Earth Expo huko Windhoek, Namibia, Oktoba 28, 2023. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

WINDHOEK – Kutoka maonesho ya bidhaa yasiyochafua mazingira na vyakula vya oganiki hadi vitu vya kisanii, Maonyesho ya "Living Earth Expo" ambayo yamejumuisha waonyeshaji bidhaa wapatao 50 wakionyesha miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii, vifaa vya watoto wa chekechea, sanaa, afya, bidhaa za mitumba, nishati mbadala na vifaa vya suluhu za kijani, yamefanyika katika mji mkuu wa Namibia, Windhoek siku ya Jumamosi yakilenga kuhimiza kwa kina ulinzi wa mazingira na maendeleo endelevu.

Selma Nasheya, mratibu wa maonyesho hayo, amesema maonyesho hayo yaliyofanyika kwa siku moja yamewakutanisha pamoja watu binafsi, mashirika na jamii ili kuongeza mawasiliano, kupata fursa ya kujifunza na kushirikiana, na kuweka msingi wa ujenzi wa mustakabali endelevu.

"Maonyesho haya bunifu ya jumuiya yamelenga kuongeza shauku ya pamoja ya kulinda Sayari ya Dunia na kufanya kazi kuelekea mustakabali safi na wenye afya kwa wote nchini Namibia," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano.

Waonyeshaji wameona maonyesho hayo kama kichocheo cha mabadiliko, na kuwawezesha watu walioshiriki kuchukua hatua zinazofanya kazi kuelekea mustakabali endelevu.

Kwa Tjakomeya Kahuika, mwanafunzi wa darasa la tisa na sehemu ya wahusika wa Woodie's Creations, mradi wa ujasiriamali katika Shule ya Waldorf huko Windhoek, maonyesho hayo yametimiza ndoto yake ya kuonyesha talanta yake kwa umma kwenye jukwaa kubwa zaidi.

"Kwa kuwa hapa, tunatoa mfano kwa vijana wengine kutengeneza fursa mpya na kushiriki kile tunachounda kupitia kazi ya pamoja," amesema.

Watu walioshiriki kwenye maonyesho hayo pia wamepata fursa ya kushiriki katika mijadala yenye ufahamu na kushuhudia maonyesho ambayo yanaangazia changamoto kubwa za mazingira na kupendekeza suluhisho.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha