Lugha Nyingine
Mkutano wa Kazi ya Mambo ya Fedha ya Kamati Kuu watoa mwelekeo wa maendeleo ya mambo ya fedha ya China
Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kazi ya mambo ya fedha ya kamati kuu uliofanyika Beijing, China. (Xinhua/Ju Peng)
Beijing - Mkutano wa kazi ya mambo ya fedha ya Kamati Kuu umefanyika Beijing kuanzia Jumatatu hadi Jumanne, ambapo Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) alitoa hotuba muhimu ambayo imechambua hali inayokabili maendeleo yenye ubora wa juu ya sekta ya mambo ya fedha na kupanga kazi husika kwa kipindi cha sasa na kijacho.
Mkutano huo umesisitiza kuwa, China itaendelea kufuata kithabiti njia ya maendeleo ya mambo ya fedha yenye umaalum wa China na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu ya sekta ya mambo ya fedha ili kutoa uungaji mkono wa dhati wa kuijenga China kwa pande zote kuwa nchi yenye nguvu na kufanikisha ustawishaji wa taifa hilo kupitia maendeleo ya mambo ya kisasa ya China.
Mkutano huo umesema kuzuia na kupunguza hatari za kifedha lazima kuendelee kuwa suala la kudumu la sekta ya mambo ya fedha, na uvumbuzi na maendeleo ya mambo ya fedha vinapaswa kuelekezwa na soko na kuendelea kufuata na kutilia maanani utekelezaji wa sheria.
Mkutano umesisitiza umuhimu wa kuimarisha mageuzi ya miundo ya upande wa utoaji katika sekta ya fedha, kuratibu ufunguaji mlango wa sekta ya mambo ya fedha na usalama wake, na kushikilia mwongozo wa jumla wa kuifanya sekta hiyo iendelee kwa utulivu huku kukiwa na maendeleo mazuri.
Mkutano huo pia umeeleza kuwa bado kuna matatizo katika sekta ya mambo ya fedha, baadhi yao ni makubwa, kama vile rushwa, ambayo yanaitaka nchi ya China kutatua matatizo hayo kimsingi.
Mkutano huo umehimiza kufanya juhudi kubwa za kuweka mazingira mazuri ya kisera na mambo ya fedha, huku kukiwa na kuongeza huduma bora za kifedha kwa mikakati mikuu, maeneo muhimu na yale yenye udhaifu. Mkutano umesisitiza kuwa sera ya mambo ya fedha yenye umakini mkubwa inapaswa kudumishwa.
Huku ukitoa wito wa juhudi za kuwezesha uwekezaji na mambo ya fedha ya kuvuka mipaka, mkutano huo umesema ushindani na ushawishi wa Mji wa Shanghai ukiwa kituo cha kimataifa cha mambo ya fedha unapaswa kuboreshwa, huku hali ya Hong Kong ikiwa kituo cha mambo ya fedha cha kimataifa iendelezwe na kuimarishwa.
Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kazi ya mambo ya fedha ya kamati kuu uliofanyika Beijing, China. (Xinhua/Yan Yan)
Habari ya picha ya wanandoa wapanda msitu katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
Mandhari ya majira ya Mpukutiko katika Kaunti ya Gongbo'Gyamda mjini Nyingchi, Mkoa wa Tibet, China
Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika lafanyika nchini Benin
Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Milima ya Altun katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma