Mabaki ya kiakilojia ya meli ya kale iliyopata ajali yafunua utukufu wa Njia ya Hariri ya Baharini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2023

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe iliyotolewa na Idara ya Taifa ya Urithi wa Utamaduni ya China (NCHA) ikionyesha mandhari ya mabaki ya meli ya kale iliyopata ajali chini ya maji kutoka Enzi ya Yuan (1271-1368) karibu na Kisiwa cha Shengbeiyu kilichoko Mji wa Zhangzhou, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. (NCHA/Xinhua)

FUZHOU - Zaidi ya miaka 700 iliyopita, meli iliyokuwa imesheheni vyombo vya kauri ilizama karibu na maji ya ufukwe wa Mkoa wa Fujian Mashariki mwa China ilipokuwa njiani kwenda nchi za ng'ambo na mabaki ya meli hiyo ya kale iliyopata ajali chini ya maji karibu na Kisiwa cha Shengbeiyu katika mji wa Zhangzhou yamefukuliwa hivi karibuni katika mradi wa uchimbuaji wa kiakiolojia, ikiwasilisha kwa Dunia ustawi wa kihistoria wa Njia ya Hariri ya Baharini wakati wa enzi hiyo.

Ufukuaji huo, ambao ulianza Mwezi Septemba mwaka jana na kudumu hadi mwezi huu, umefanywa kwa pamoja na Kituo cha Taifa cha Akiolojia cha China (NCA), taasisi ya utafiti ya akiolojia ya Mkoa wa Fujian na idara ya utamaduni na utalii ya manispaa ya Zhangzhou.

Yakiwa yanapatikana kwenye makutano ya njia ya mashariki na njia ya kusini ya Njia ya Kale ya Hariri ya Baharini, maji ya bahari karibu na Kisiwa cha Shengbeiyu ni eneo linalotokea ajali za vyombo vya majini mara kwa mara kwa kuwa limezungukwa na miamba na lina hali ngumu ya bahari.

Meli hiyo ya kale kutoka Enzi ya Yuan (1271-1368) imepatikana hapo chini ya mchanga kwenye kina cha maji chenye urefu wa karibu mita 30.

Takriban bidhaa 20,000 zimepatikana, huku mkusanyiko huo ukijumuisha vyombo zaidi ya 17,100 vya kaure za Longquan Celadon, maarufu nchini China kwa rangi zake maridadi, hasa vivuli vya kijani kibichi na samawati isiyokolea. Bakuli, sahani, vikombe na vichomea uvumba ni miongoni mwa vyombo hivyo vilivyopatikana, ambavyo inaaminika kuwa vilitengenezwa katika Enzi ya Yuan.

"Meli hiyo iliyozama ina idadi kubwa zaidi ya vyombo vya kauri Longquan vilivyopatikana hadi sasa, vikiwa mfano wa kilele cha mauzo ya nje ya Longquan katika Enzi ya Yuan," amesema Chen Hao, Naibu Mkuu wa kituo cha akiolojia cha chini ya maji cha taasisi ya utafiti wa akiolojia ya Mkoa wa Fujian.

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe iliyotolewa na Idara ya Taifa ya Urithi wa Utamaduni ya China (NCHA) ikionyesha vyombo vya kauri vikiwa ndani ya mabaki ya meli ya kale iliyopata ajali chini ya maji kutoka Enzi ya Yuan (1271-1368) karibu na Kisiwa cha Shengbeiyu kilichoko Mji wa Zhangzhou, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. (NCHA/Xinhua)

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe iliyotolewa na Idara ya Taifa ya Urithi wa Utamaduni ya China (NCHA) ikionyesha vyombo vya kauri vilivyoopolewa kutoka kwenye mabaki ya meli ya kale iliyopata ajali chini ya maji kutoka Enzi ya Yuan (1271-1368) karibu na Kisiwa cha Shengbeiyu kilichoko Mji wa Zhangzhou, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. (NCHA/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha