China yasema itaendelea na juhudi bila kuchoka kutafuta suluhu juu ya suala la Palestina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2023

BEIJING - China itaendelea kufanya juhudi bila kuchoka kwa ajili ya suluhu ya pande zote, yenye haki na ya kudumu juu ya suala la Palestina mapema, amesema Msemaji wa Wizara ya mambo ya Nje Wang Wenbin Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa juu ya Israel kusema "inakataa moja kwa moja" wito wa Umoja wa Mataifa (UN) wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza baada ya Baraza Kuu la UN kupitisha azimio kuhusu hali ya Palestina na Israel huku nchi wanachama wengi wakiliunga mkono katika kikao maalum cha dharura cha Oktoba 28.

Wang amesema azimio hilo la Baraza Kuu la UN linatoa wito wa "makubaliano ya haraka, ya kudumu na endelevu ya kusimamisha vita kwa ajili ya huduma za kibinadamu kutakakopelekea kusitishwa kwa uhasama", kufuata sheria za kimataifa, ulinzi wa raia, na kubatilisha amri ya raia kuhama kaskazini mwa Gaza. Wang amesema azimio hilo pia "linakataa majaribio yoyote ya kuwahamisha kwa lazima raia wa Palestina."

"Hii inaonyesha wito mkubwa kutoka kwa nchi nyingi duniani," Wang amesema.

"Kwa muda mrefu sana, maeneo ya Wapalestina yamekuwa yakikaliwa kiharamu. Kwa muda mrefu sana, haki ya watu wa Palestina ya kuwa na nchi huru imekuwa ikipuuzwa. Na kwa muda mrefu sana, haki zao za kimsingi hazijapata dhamana ya kimsingi," Wang amesema, huku akiongeza kuwa sababu hizi kuu za mzunguko wa migogoro kati ya Palestina na Israel na dhuluma kama hiyo ya kihistoria haipaswi kuendelea.

"Nchi zote zina haki ya kujilinda. Lakini haki hiyo inapaswa kutekelezwa kwenye msingi wa kufuata sheria za kimataifa, sheria ya kimataifa ya kibinadamu hasa na kulinda usalama wa raia," Wang amesema.

Amesema kuwa, historia inatuambia kuwa matumizi ya nguvu hayawezi kamwe kuleta amani ya kudumu na kulipiza vurugu kwa vurugu itasababisha tu mzunguko mbaya wa kulipiza kisasi.

“Njia ya kimsingi ya kumaliza suala la Palestina iko katika utekelezaji wa suluhu ya kuwepo kwa nchi mbili Palestina na Israeli za kuishi kwa amani ” ameongeza Wang. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha