Miji ya Chaozhou na Chongqing nchini China yachaguliwa kujiunga kwenye Mtandao wa Miji Bunifu wa UNESCO

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2023

Picha iliyopigwa Februari 14, 2021 ikionyesha mandhari ya Mji wa Chaozhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Liu Dawei)

Picha iliyopigwa Februari 14, 2021 ikionyesha mandhari ya Mji wa Chaozhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Liu Dawei)

PARIS – Miji ya Chaozhou na Chongqing nchini China imechaguliwa pamoja na miji mingine 53 duniani kote na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kujiunga kwenye Mtandao wa Miji Bunifu wa UNESCO (UCCN) katika Siku ya Miji Duniani iliyoadhimishwa jijini Paris, Ufaransa.

"Miji hiyo mipya imetambuliwa kwa kujitolea kwao kwa juhudi kubwa kutumia utamaduni na ubunifu kama sehemu ya mikakati yao ya maendeleo, na kuonyesha kivitendo utekelezaji wa ubunifu katika upangaji miji unaotilia maanani binadamu," UNESCO imesema Jumanne katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Chaozhou na Chongqing zimepewa hadhi ya Miji Bunifu ya Mambo ya Vyakula au Gastronomia, na ya Usanifu, mtawalia.

"Miji hiyo katika Mtandao wetu wa Miji Bunifu inaongoza njia linapokuja suala la kuimarisha ufikiaji wa utamaduni na kuhimiza nguvu ya ubunifu kwa ajili ya unyumbufu na maendeleo ya miji," Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema.

Miji hiyo mipya iliyoteuliwa itashirikiana na miji mingine ya Mtandao huo ili kuimarisha uthabiti wao katika kukabiliana na vitisho vinavyojitokeza kama vile mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa usawa, na ukuaji wa haraka wa miji. UNESCO imesema ifikapo Mwaka 2050, asilimia 68 ya idadi ya watu wote duniani wanatarajiwa kuishi mijini.

Picha hii iliyopigwa Oktoba 30, 2023 ikionyesha mandhari ya mji ya Chongqing, Kusini-Magharibi ya China. Ukiwa unapatikana sehemu za juu za Mto Yangtze, Mji wa Chongqing umeendelea kujijenga kuwa kizuizi kikubwa cha ikolojia. (Xinhua/Wang Quanchao)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha