Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akutana na mwenzake wa Honduras, Eduardo Reina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 02, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Y akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Honduras Eduardo Reina mjini Beijing, China, Novemba 1, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Honduras Eduardo Reina mjini Beijing, China, Novemba 1, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na mwenzake wa Honduras Eduardo Reina mjini Beijing, China siku ya Jumatano ambapo amesema kuwa uhusiano kati ya China na Honduras umeendelea kwa kasi chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, ukionyesha matarajio mapana na nguvu kubwa ya uhai tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano ya kidiplomasia.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema kuwa, China inasifu sana Honduras kushikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, inaunga mkono juhudi za Honduras za kulinda mamlaka ya nchi na kuhimiza maendeleo yake, na inaiunga mkono Honduras katika kuchagua kwa kujiamulia njia ya maendeleo inayoendana na hali ya nchi yake.

Wang ameikaribisha Honduras kushiriki kwenye Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) ikiwa Nchi Mgeni wa Heshima. Wang ameitakia nchi hiyo mafanikio kamili kwenye maonesho hayo, na amesema kuwa China iko tayari kutoa fursa zaidi kwa bidhaa za Honduras kuingia China.

“China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na Honduras na kulinda maslahi halali ya nchi zinazoendelea na haki na usawa wa kimataifa. China iko tayari kushirikiana na Honduras ili kuboresha Jukwaa la China na Nchi za Latin Amerika na kuleta ushirikiano wa jumla kati ya China na Latin Amerika katika ngazi mpya.”

Kwa upande wake Reina ameishukuru China kwa kuialika Honduras kushiriki Maonyesho ya 6 ya CIIE ikiwa Nchi Mgeni wa Heshima, akisema kwamba ingawa uhusiano wa nchi hizo mbili ulianza kwa kuchelewa, una mustakabali mzuri.

Amesisitiza kuwa Honduras itafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inathamini sana mfululizo wa mipango muhimu iliyopendekezwa na China. Amesema Honduras iko tayari kushiriki pamoja na China katika ujenzi wa kiwango cha juu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha