

Lugha Nyingine
Bolivia yatangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel
(CRI Online) Novemba 02, 2023
Serikali ya Bolivia imetangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel kufuatia mashambulizi ya Israel dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Bolivia Bibi María Prada, amesema Jumanne wiki hii, kwamba kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, serikali ya Bolivia imeamua kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel, pia inapanga kutoa msaada wa kibinadamu kwa waathirika wa mapigano kati ya Palestina na Israel.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma