Uvumbuzi wawa ajenda ya kipaumbele kwenye kongamano la kimataifa la mabadiliko ya tabianchi mjini Vienna, Austria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 03, 2023

Watu wakihudhuria kongamano la kimataifa la nishati na mabadiliko ya tabianchi mjini Vienna, Austria, Novemba 2, 2023. (Xinhua/Liu Xinyu)

Watu wakihudhuria kongamano la kimataifa la nishati na mabadiliko ya tabianchi mjini Vienna, Austria, Novemba 2, 2023. (Xinhua/Liu Xinyu)

VIENNA - Kongamano la Kimataifa la Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi la Vienna Mwaka 2023 ambalo linawakutanisha pamoja wafanya maamuzi waandamizi, wataalam wa kimataifa na wadau wengine kujadili njia bunifu za kuongeza kasi ya kuhamia kwenye nishati mpya, na kuhimiza hatua ya mabadiliko ya tabianchi duniani, limeanza mjini Vienna, Austria siku ya Alhamisi likiwa na kaulimbiu isemayo "Maendeleo kwa uvumbuzi".

Kongamano hilo la siku mbili pia litatoa taarifa katika mkutano ujao wa 28 wa Nchi Watia saini kwa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), waandaaji wake wamesema.

Rais wa Austria Alexander Van der Bellen amesema katika hafla ya ufunguzi kwamba kabla ya COP28, kongamano hilo "linaweza kutumika kama fursa ya kusisitiza uharaka wa kuchukua hatua za kuleta suluhu zenye uvumbuzi za kijani katika sekta ya nishati na kujenga miungano."

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Gerd Mueller amesema: "Tunahitaji mtindo mpya wa kimataifa ulio endelevu, na wa haki wa ukuaji na utandawazi wa kiuchumi. Hiyo ina maana ya kuzalisha zaidi kwa kutumia nishati kidogo na rasilimali chache, na kutoa hewa chafuzi chache. Tutajadili na kuonyesha suluhu madhubuti za mageuzi ya kijani ili kulinda tabianchi, watu, na sayari ya dunia kwa vizazi vijavyo."

Shughuli zaidi ya 50 zitafanyika pembezoni mwa kongamano hilo linaloandaliwa kwa pamoja na UNIDO, serikali ya Austria na Taasisi ya Kimataifa ya Uchambuzi wa Mifumo ya Matumizi. Siku ya Ijumaa, Shirika la Maendeleo na Ushirikiano wa Nishati Duniani, shirika lenye makao yake makuu mjini Beijing, China linalojishughulisha na maendeleo ya nishati endelevu, litakuwa mwenyeji wa shughuli ya pembezoni ya "Maendeleo ya Tabianchi kwa mustakabali endelevu" pamoja na Shirika la Hali ya Hewa Duniani na kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei.

Watu wakihudhuria kongamano la kimataifa la nishati na mabadiliko ya tabianchi mjini Vienna, Austria, Novemba 2, 2023. (Xinhua/Liu Xinyu)

Watu wakihudhuria kongamano la kimataifa la nishati na mabadiliko ya tabianchi mjini Vienna, Austria, Novemba 2, 2023. (Xinhua/Liu Xinyu)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha