Rais Xi Jinping atuma barua kwa Maonyesho ya 6 ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), na kuahidi kufungua mlango kwenye kiwango cha juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 06, 2023

Rais wa China Xi Jinping ametuma barua kwa Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), ambayo yamefunguliwa mjini Shanghai siku ya Jumapili, na kuahidi juhudi madhubuti za kuhimiza kufungua mlango kwenye kiwango cha juu.

Yakiwa yalifanyika kwa mara ya kwanza Mwaka 2018, maonyesho hayo ya kila mwaka yametumia fursa ya soko kubwa la China, yametimiza kazi yake ya kuwa jukwaa la manunuzi ya kimataifa, uhamasishaji wa uwekezaji, mawasiliano kati ya watu, uwazi na ushirikiano, na kutoa mchango wa hamasa katika kuunda muundo mpya wa maendeleo na kuendeleza maendeleo ya uchumi wa Dunia, Rais Xi amesema katika barua hiyo.

Rais Xi amedhihirisha kuwa kuimarika kwa uchumi wa dunia kunakosa kasi na kunahitaji mshikamano na ushirikiano wa nchi zote, amesema China daima itakuwa fursa muhimu kwa maendeleo ya Dunia.

Ameahidi kuwa China itahimiza kwa uthabiti kufungua mlango kwenye kiwango cha juu na kuendelea kuufanya utandawazi wa uchumi kuwa wazi, jumuishi, wenye uwiano na manufaa zaidi kwa wote.

CIIE ni maonyesho ya kwanza duniani ya ngazi ya kitaifa yanayolenga uagizaji wa bidhaa kutoka nje, na ni maonesho makubwa uliopendekezwa, kupangwa, kuhamasishwa na kuhimizwa na Rais Xi mwenyewe.

Tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2018, maonyesho hayo yamekuwa sehemu ya China kuonyesha dhana mpya ya maendeleo, jukwaa la ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na bidhaa ya kiumma kwa Dunia nzima.

Maonyesho matano yaliyopita yalipokea nchi na mashirika ya kimataifa jumla ya 131 kushiriki kwenye maonyesho hayo, ambapo bidhaa mpya, teknolojia mpya na huduma mpya karibu 2,000, zikionekana kwa mara ya kwanza, na thamani ya makubaliano ya mauzo ya jumla kufikia karibu dola bilioni 350 za Kimarekani.

Maonyesho hayo ya mwaka huu, yaliyopangwa kufanyika kuanzia Novemba 5 hadi 10, yameweka rekodi mpya huku kampuni 289 kati ya Kampuni 500 Bora Duniani na viongozi wa sekta ya biashara wameshiriki kwenye maonesho hayo. Kampuni zaidi ya 3,400 na wageni wa kitaalamu 394,000 wamejiandikisha kushiriki kwenye maonyesho hayo, hali ambayo imerudi kwenye viwango vya kabla ya janga UVIKO-19.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha