

Lugha Nyingine
Maonyesho ya CIIE ya China yatambuliwa kimataifa kwa kuendeleza maendeleo na ushirikiano
Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), yaliyoanza mjini Shanghai siku ya Jumapili yamepongezwa na viongozi na maofisa wa nchi mbalimbali kwa mchango wake wa kutoa fursa za biashara kwa kampuni za kimataifa, kuendeleza biashara na ushirikiano wa kimataifa, na pia maendeleo ya kiuchumi duniani.
Waziri Mkuu wa Australia Bw. Anthony Albanese amesema Australia na China zimenufaika kutokana na maendeleo na utulivu wa kikanda, na kuwa biashara ya bidhaa na huduma kati ya pande mbili imeongezeka karibu maradufu tangu Mkataba wa Biashara Huria kati ya China na Australia ulipoanza kutekelezwa Mwaka 2015.
Waziri Mkuu wa Cuba Bw. Manuel Marrero Cruz amesema Cuba inatilia maanani sana na inashiriki mara kwa mara katika maonesho hayo muhimu, na kusema kufanyika kwa maonesho hayo kutasaidia jumuiya ya kimataifa kuharakisha uimarikaji wa uchumi wa dunia na maendeleo ya biashara.
Viongozi wengine kutoka Kazakhstan, Serbia, Afrika Kusini na Iran pia wameyapongeza maonesho hayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma