Rais Xi Jinping akutana na makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Paul Mashatile

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 07, 2023

Rais wa China Xi Jinping akikutana na makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Novemba 6, 2023. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Novemba 6, 2023. (Xinhua/Ding Haitao)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile mjini Beijing siku ya Jumatatu ambapo amesema mwaka huu ni maadhimisho ya kutimia miaka 25 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika Kusini, huku uhusiano wa pande mbili ukiingia katika "zama ya dhahabu."

Katika ziara yake ya nne nchini Afrika Kusini Mwezi Agosti, mwaka huu, Rais Xi na Rais Cyril Ramaphosa walikubaliana kuwa China na Afrika Kusini zinapaswa kuwa washirika wa kimkakati wa kuaminiana kwa kiwango cha juu, washirika wa maendeleo wanaotafuta maendeleo kwa pamoja, washirika wa kirafiki wanaofurahia maelewano, na washirika wa kimataifa wa kulinda haki. "China iko tayari kufanya kazi na Afrika Kusini ili kuendelea kuimarisha uhusiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika Kusini na kuupeleka uhusiano huo uendelee kwenye ngazi mpya," Rais Xi amesema.

Rais Xi amesema kuwa China inaiunga mkono Afrika Kusini katika kutafuta njia ya maendeleo ya kisasa inayoendana na hali yake ya nchi, na China iko tayari kuimarisha zaidi msingi wa kuaminiana kisiasa na kuinua kiwango cha ushirikiano wa kunufaishana na Afrika Kusini.

Rais Xi pia ameeleza nia ya China ya kushirikiana na Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika katika kutekeleza mipango mitatu ya China ya kuunga mkono maendeleo ya viwanda, kilimo cha kisasa na maendeleo ya vipaji vya Afrika, pamoja na hatua nane za kuunga mkono ushirikiano wa kiwango cha juu wa ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kutekeleza miradi ya ushirikiano ya kiwango cha juu na endelevu inayonufaisha maisha ya watu, kufanya kazi kwa ajili ya ushirikiano wa kimkakati na endelevu kati ya China na Afrika, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi pia ametoa wito kwa pande hizo mbili kuendelea kushirikiana kwa karibu ndani ya mfumo wa BRICS, kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, na kuhimiza mfumo wa usimamizi wa dunia kuendelea kwa mwelekeo unaofaa kwa nchi zinazoendelea.

Kwa upande wake Mashatile amesema ziara ya Rais Xi nchini Afrika Kusini yenye mafanikio mnamo Mwezi Agosti mwaka huu iliimarisha zaidi urafiki wa jadi kati ya Afrika Kusini na China, na kutia msukumo mkubwa katika maendeleo ya baadaye ya uhusiano.

Upande wa Afrika Kusini unatarajia kuimarisha muunganisho kati ya mkakati wake wa maendeleo na Pendekezo la China la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kuendelea kuzidisha ushirikiano wa kivitendo katika nyanja mbalimbali.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Novemba 6, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Novemba 6, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha