Rais Xi Jinping atoa wito wa kuruhusu intaneti kunufaisha watu wa nchi zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 09, 2023

Rais Xi Jinping wa China akihutubia kwa njia ya video Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani wa Mwaka 2023 (WIC), Novemba 8, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China akihutubia kwa njia ya video Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani wa Mwaka 2023 (WIC), Novemba 8, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatano akihutubia kwa njia ya video ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani wa Mwaka 2023 (WIC) ametoa wito wa kuruhusu mtandao wa intaneti kunufaisha zaidi watu wa nchi zote na kwamba maono yake ya kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwenye nafasi za mtandao wa intaneti, ambayo aliyapendekeza katika WIC ya pili Mwaka 2015, yamepata kutambulika kimataifa na kupata mwitikio.

Rais Xi amesema, maono hayo yanajibu maswali ya zama zetu kuhusu kupunguza pengo la maendeleo, kukabiliana na changamoto kwa usalama, na kuimarisha kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbali tofauti.

Amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inahitaji kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa kivitendo ili kuendeleza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja katika nafasi za mtandao wa intaneti kwenye ngazi mpya.

Ametoa wito wa kutoa kipaumbele kwa maendeleo ili kuruhusu matunda ya maendeleo ya mtandao wa intaneti kunufaisha nchi nyingi zaidi na watu wao.

Rais Xi amesisitiza haja ya kuboresha ufikiaji wa kiumma kwa huduma zinazotegemea habari, kupunguza pengo la kidijitali, na kuboresha maisha ya watu kwa kutumia maendeleo ya mtandao wa intaneti.

Rais Xi akitoa mwito wa kujenga nafasi za mtandao wa intaneti zilizo za amani na usalama zaidi, amesisitiza haja ya kuheshimu uhuru wa nafasi za mtandao wa intaneti na njia ya kila nchi ya usimamizi wa intaneti na haja ya kupinga umwamba, mapambano ya kambi na mashindano ya silaha katika nafasi za mtandao wa intaneti.

Ameendelea kusisitiza haja ya kukabiliana na uhalifu wa mtandaoni, kuimarisha usalama wa data na ulinzi wa habari za kibinafsi, na kukabiliana ipasavyo na hatari na changamoto zinazoletwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa sheria, jamii na maadili.

"China iko tayari kushirikiana na pande zote kutekeleza Pendekezo la Usimamizi wa Teknolojia za Akili Bandia Duniani na kuhimiza maendeleo salama ya AI (Teknolojia za Akili Bandia)," Rais Xi amesema.

Rais Xi Jinping wa China akihutubia kwa njia ya video Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani wa Mwaka 2023 (WIC), Novemba 8, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

Rais Xi Jinping wa China akihutubia kwa njia ya video Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani wa Mwaka 2023 (WIC), Novemba 8, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha