Shirikisho la Waandishi wa Habari la China latoa Wimbo wa Hamasa kwa Waandishi wa Habari wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 09, 2023

Katika siku inayoangukia Sikukuu ya 24 ya Waandishi wa Habari ya China ambayo huadhimishwa Tarehe 8, Novemba kila mwaka, Shirikisho la Waandishi wa Habari la China limetoa wimbo rasmi wa hamasa kwa ajili ya waandishi wa habari wa China, “Jina Langu”, ambao umechapishwa kwenye majukwaa mbalimbali ya mtandaoni ya China na kupata mwitiko mzuri kutoka kwa jamii.

Inafahamika kuwa wimbo huo umeimbwa na waandishi wengi wa habari wa mstari wa mbele pamoja na waimbaji vijana. Kwa kutumia mistari ya mashairi ya kuvutia na tuni inayogusu moyo, wimbo huo unaonesha dhahiri safari ya waandishi wa habari wa China wakishikilia maadili ya kitaaluma, na kuonesha kikamilifu namna waandishi wa habari wa China wanavyorekodi hali halisi ya wakati kwa kutumia maandishi na lenzi za kamera, hisia na dhamira ya asili ya kulinda haki na usawa na kufuatilia maadili ya uandishi wa habari.

Kwa sasa shirikisho la waandishi wa habari la China kwa wakati mmoja limetoa kwa umma karatasi ya muziki na mistari ya mashairi ya wimbo huo, ili kuwawezesha waandishi wa habari wa watu wengine kuuimba. Katika karatasi hiyo ya muziki, mtunzi wa muziki huo ameunganisha muziki wa kisasa na kaulimbiu ya wimbo huo, akiwasilisha kwa umma muziki mzuri wenye sifa ya kijadi na pia hisia ya kisasa.

Karatasi ya muziki ya wimbo "Jina langu"

Karatasi ya muziki ya wimbo "Jina langu"

Karatasi ya muziki ya wimbo "Jina langu"

Karatasi ya muziki ya wimbo "Jina langu"

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha