Rais Xi Jinping aipongeza Cambodia kwa kuadhimisha miaka 70 tangu kupata uhuru

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2023

Beijing - Rais wa China Xi Jinping ameipongeza Cambodia kwa kuadhimisha miaka 70 tangu ipate uhuru wake, katika salamu zake za pongezi kwa Mfalme wa Cambodia Norodom Sihamoni siku ya Alhamisi, amesema kuwa watu wa Cambodia wamejitolea kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi yao na wamepata mafanikio mapya kila wakati kwenye ujenzi wa nchi katika miaka ya hivi karibuni.

"Ikiwa ni nchi jirani rafiki wa jadi, China, kama ilivyofanya siku zote, itaiunga mkono Cambodia kwa uthabiti katika kudumisha utulivu, kuhimiza maendeleo na kuboresha maisha ya watu," Rais Xi amesema.

Huku akieleza kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Cambodia na Mwaka wa Urafiki kati ya China na Cambodia, Rais Xi amekumbuka kuwa yeye na Mfalme Sihamoni walikutana Beijing na Hangzhou mwaka huu ili kuweka dira ya jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi amesema anatilia sana maanani maendeleo ya uhusiano kati ya China na Cambodia na atashirikiana na Mfalme Sihamoni katika kuimarisha mwongozo wa kimkakati wa uhusiano wa pande mbili, ili kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja iliyo ya sifa bora ya juu, kiwango cha juu na kigezo cha juu katika zama mpya.

Siku hiyo hiyo, Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alituma salamu za pongezi kwa Samdech Techo Hun Sen, Mkuu wa Chama cha Umma cha Cambodia. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha