Shughuli ya ukaribisho wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuja China kwa Okestra ya Philadelphia ya Marekani yafanyika Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2023

Shughuli ya ukaribisho wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuja China kwa Okestra ya Philadelphia ya Marekani imefanyika Beijing jana Alhamisi, tarehe 9, ambapo wadau karibu 100 wa China na Marekani wa sekta mbalimbali walihudhuria kwenye shughuili hiyo.

Yang Wanming, Mkuu wa Shirikisho la watu wa China kwa Urafiki wa nchi za kigeni kwenye hotuba yake amesema, miaka 50 iliyopita Okestra ya Philadelphia ilifanya ziara ya kihistoria nchini China kwa mara ya kwanza na kuwa kundi maarufu la kwanza la watumbuizaji wa muziki la Marekani kutumbuiza nchini China baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

Amesema hii ilikuwa “ziara ya kuvunja barafu ya Sanaa” ya China na Marekani, na ilitoa mchango mkubwa katika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili. Amesema, katika miaka 50 iliyopita, Okestra hiyo imefanya ziara China mara 12, ikihimiza mawasiliano kati ya watu kwa kutumia muziki.

Balozi wa Marekani nchini China R. Nicholas Burns kwenye hotuba yake amesema, Okestra ya Philadelphia imetoa mchango mkubwa katika mabadilishano ya kitamaduni kati ya China na Marekani.

Amesema, katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, siyo tu okestra hiyo imeleta burudani yake kwa China, bali pia imewaalika wasanii wa China kujiunga nayo, na imeanzisha ushirikiano wa muda mrefu na wenye mtazamo wa mbali na taasisi husika za China. Anaamini chini ya juhudi zinazoendelea, mabadilishano na mawasiliano kati ya nchi hizo mbili yataendelea kuimarishwa zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha