Kundi la madaktari wa China visiwani Zanzibar wafanya upasuaji wa kwanza wa kineli cha nyongo yenye jeraha dogo (MIS)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2023

Kiongozi wa kundi la 33 la madaktari wa China wanaotoa msaada visiwani Zanzibar, Tanzania Jiang Guoqing (kwanza kushoto) akifanya upasuaji wa mgonjwa wa Zanzibar hivi karibuni. (Picha kwa hisani ya kundi hilo la madaktari)

Kiongozi wa kundi la 33 la madaktari wa China wanaotoa msaada visiwani Zanzibar, Tanzania Jiang Guoqing (kwanza kushoto) akifanya upasuaji wa mgonjwa wa Zanzibar hivi karibuni. (Picha kwa hisani ya kundi hilo la madaktari)

Jiang Guoqing, ambaye ni kiongozi wa kundi la 33 la madaktari wa China wanaotoa msaada visiwani Zanzibar, Tanzania hivi karibuni amefanya kwa mafanikio upasuaji wa kineli cha nyongo yenye jeraha dogo kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja ya Zanzibar, ambao umesaidia mgonjwa mwanamke visiwani humo kupoza maumivu yake.

Daktari Jiang anatilia maanani kufundisha madaktari wa Zanzibar mafunzo ya kufanya upasuaji. Akijua kuwa daktari Rashid wa hospitali hiyo bado hajaelewa teknolojia husika, Jiang alimfafanulia kila hatua wakati wa kufanya upasuaji huo.

Rashid amesema, “Ninawashukuru madaktari wa China waliokuja hapa kutoka mbali. Wamenifundisha ujuzi mwingi na ni mfano mzuri kwangu mimi kujifunza kutoka kwao. Hakika nitajifunza ujuzi wa udaktari siku zijazo, na kutumia ujuzi bora wa matibabu kusaidia wagonjwa wengi zaidi.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha