Lugha Nyingine
Rais wa China ahudhuria na kuhutubia hafla ya kukaribisha ziara yake iliyoandaliwa na vikundi vya urafiki nchini Marekani
Rais Xi Jinping wa China leo amehudhuria na kuhutubia tafrija ya kukaribisha ziara yake iliyofanyika mjini San Francisco ambayo iliandaliwa kwa pamoja na vikundi vya urafiki nchini Marekani.
Katika hotuba yake, rais Xi amesema kuishi kwa pamoja kwa amani ni msingi wa uhusiano wa kimataifa, na pia ni msingi unaopaswa kushikiliwa kithabiti na China na Marekani, na kwamba haipaswi kuichukulia China ambayo inashikilia kujiendeleza kwa njia ya amani kama tishio.
Pia amesema kuwa kuheshimiana ni nidhamu na msingi kwa mawasiliano ya watu, vilevile ni kanuni ya kimsingi kwa mawasiliano kati ya China na Marekani. China inaheshimu njia ya Marekani ya kujiendeleza na mfumo wake wa jamii, na njia ya Ujamaa wenye Umaalumu wa China inaongozwa na nadharia ya kisayansi ya ujamaa, na mizizi yake imejikita kwenye utamaduni wa China wenye historia ya zaidi ya miaka elfu tano. Amesema njia hizi mbili ni tofauti, lakini zote ni chaguo la wananchi na kuonesha thamani ya pamoja ya binadamu wote, na zote zinatakiwa kuheshimiwa.
Rais Xi amesisitiza kuwa, matumaini ya uhusiano kati ya China na Marekani yapo kati ya wananchi na mustakabali unategemea vijana, na watu wa sekta mbalimbali za Marekani wanakaribishwa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma