Waandishi wa habari wa kimataifa watembelea kupata uzoefu katika eneo la kibiashara lenye historia ya karne nyingi mjini Shenzhen, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 16, 2023

Mtaa Mkongwe wa Dongmen, ulioanzia katikati ya Enzi ya Ming ya China ya kale (1368-1644), ambao ni eneo kongwe zaidi la kibiashara katika Mji wa Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini Mashariki mwa China.

Kabla ya Shenzhen kuanzishwa kuwa mji, jina la "Shenzhen" ililiita tu eneo la Dongmen, ambalo hapo awali liliitwa Soko Kongwe la Shenzhen. Mwaka 1979, baada ya kuanzishwa kuwa mji kwa Shenzhen, eneo hilo lilipewa jina la Mtaa Mkongwe wa Dongmen.

Mwezi Desemba 2022, serikali ya Mji wa Shenzhen ilianzisha ukarabati na uboreshaji wa Mtaa Mkongwe wa Dongmen. Mradi huo unalenga kuchanganya urithi wa kitamaduni na biashara na viwanda, kujenga mustakabali wa eneo hilo kongwe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha