Kongamano la kujadili njia za kisasa kwa China na Afrika lafanyika nchini Kenya

(CRI Online) Novemba 16, 2023

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Wawakilishi kutoka China na Kenya wamehudhuria kongamano la kujadili njia zinazowezekana kwa ajili ya China na nchi za Afrika kuwa za kisasa.

Kongamano hilo lililofanyika jijini Nairobi, Kenya, chini ya kaulimbiu “Njia za Usasa kwa China na Nchi za Afrika,” limevutia washiriki kadhaa wakiwemo wanadiplomasia, wasomi, na wanahabari, na lilionyesha hamu ya China na Afrika kutimiza maendeleo ya utulivu na jumuishi.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti na Mipango ya Taasisi ya Historia ya Chama na Nyaraka Muhimu chini ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Zhang Peng, amesema njia ya kisasa ya China ni njia inayoelekea maendeleo ya China, ikihusu manufaa ya pamoja na kunufaishana.

Naye rais wa Taasisi ya Sera ya Afrika, Peter Kagwanja, amesema zikiwa na historia ya ukoloni, China na Afrika zimeungana katika nia yao ya kujitafutia njia ya maendeleo inayoendana na mazingira yao ya kipekee.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha