Waziri wa Mambo ya Nje wa China aeleza kuhusu mkutano wa viongozi wa China na Marekani, ushiriki wa Rais Xi katika Mkutano wa 30 wa Viongozi wa APEC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2023

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba   ya “Kushikilia Lengo la Kuanzishwa kwa APEC, Kuimarisha Mshikamano na Ushirikiano, na Kuhimiza kwa Pamoja Ukuaji wa Uchumi wenye Ubora wa Juu katika Eneo la Asia-Pasifiki” kwenye mkutano wa 30 wa Viongozi wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) mjini Francisco, Marekani, Novemba 17, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amejulisha hali kwa waandishi wa habari siku ya Jumamosi kuhusu mazungumzo ya Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Marekani Joe Biden na kuhudhuria kwake Mkutano wa 30 wa Viongozi wa APEC huko San Francisco, ambapo Wang amesema inaaminika kuwa ziara ya Rais Xi imevutia ufuatiliaji makini wa Dunia, hali ambayo imeongeza utulivu kwenye uhusiano kati ya China na Marekani, imeleta msukumo mpya kwenye ushirikiano wa Asia na Pasifiki na kuingiza nishati chanya katika mazingira ya kimataifa na kikanda

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameeleza kuwa, Rais Xi alisema huko San Francisco kwamba, China na Marekani zinapaswa kuwa na maono mapya, akisisitiza kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kuendeleza kwa pamoja mtazamo sahihi, kushughulikia migongano kwa pamoja na kwa ufanisi, na kuthamini kanuni na mistari myekundu ya kila mmoja wao, kuendeleza kwa pamoja ushirikiano wa kunufaishana, kubeba kwa pamoja majukumu ya nchi kubwa na kuhimiza kwa pamoja mawasiliano kati ya watu.

Akithibitisha ahadi tano alizozitoa kwenye mkutano wa Bali, Rais Biden alisema kuwa Marekani haitafuti vita baridi vipya, haitafuti kubadili mfumo wa China, haitafuti kujenga miungano ya nchi na kambi dhidi ya China, haiungi mkono "kujitenga kwa Taiwan," na kwamba haina nia ya kuwa na mgogoro na China, Wang amesema.

Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Joe Biden wakitembea baada ya mazungumzo yao katika eneo la Filoli Estate lililoko Jimbo la California, Marekani, Novemba 15, 2023. (Xinhua/Rao Aimin)

Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Joe Biden wakitembea baada ya mazungumzo yao katika eneo la Filoli Estate lililoko Jimbo la California, Marekani, Novemba 15, 2023. (Xinhua/Rao Aimin)

Wang ametaja matokeo muhimu yaliyofikiwa katika mkutano huo, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kikundi kazi cha ushirikiano wa kukabiliana na dawa za kulevya na makubaliano ya kuanza tena, kwa misingi ya usawa na heshima, mawasiliano ya ngazi ya juu na mazungumzo ya kitaasisi kati ya majeshi ya nchi hizo mbili, na kuhimiza kwa pamoja mafanikio ya Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini (COP28) kwa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi huko Dubai.

Katika ziara hiyo, Rais Xi alialikwa kwenye tafrija ya ukaribisho iliyoandaliwa kwa pamoja na mashirika ya kirafiki nchini Marekani, ambapo alitoa hotuba muhimu, akisisitiza kuwa msingi wa uhusiano kati ya China na Marekani umewekwa na watu wa pande hizo mbili.

Kuhusu jinsi ya kujenga "miaka 30 ya dhahabu" ijayo katika eneo la Asia-Pasifiki, Rais Xi ametoa wito wa kutafuta maendeleo yanayotokana na uvumbuzi, ya uwazi, ya kijani, na ambayo ni jumuishi yanayoleta manufaa kwa wote.

Picha iliyopigwa Novemba 12, 2023 ikionyesha mabango ya APEC 2023 mbele ya Kituo cha Kimataifa cha Vyombo vya Habari cha APEC 2023 huko San Francisco, Marekani. (Xinhua/Li Rui)

Picha iliyopigwa Novemba 12, 2023 ikionyesha mabango ya APEC 2023 mbele ya Kituo cha Kimataifa cha Vyombo vya Habari cha APEC 2023 huko San Francisco, Marekani. (Xinhua/Li Rui)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha