

Lugha Nyingine
Idadi ya vifo vya Wapalestina huko Gaza yazidi 13,000
Watu wa Palestina wanaonekana wakiwa njiani kutoka Mji wa Gaza kuelekea Kusini katika eneo la Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 18, 2023. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)
GAZA - Ofisi ya vyombo vya habari ya serikali ya Gaza imetangaza Jumapili kwamba idadi ya vifo vya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza imezidi 13,000 tangu mapigano kati ya Israel na Kundi la Hamas kuzuka Oktoba 7.
Mkurugenzi Mkuu wa ofisi hiyo ya vyombo vya habari Ismail al-Thawabta amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa miongoni mwa waliofariki ni watoto 5,500 na wanawake 3,500, na wengine zaidi ya 30,000 walijeruhiwa.
Al-Thawabta amesema idadi ya watu ambao hawajulikani walipo imepita 6,000, wakiwemo watoto na wanawake 4,000 ambao bado wako chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya Israel.
Israel imekuwa ikifanya mashambulizi huko Gaza katika muda wa wiki kadhaa zilizopita kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya kushtukiza ya Kundi la Hamas katika eneo la Kusini mwa Israel yaliyofanywa Oktoba 7, ambapo wanamgambo wa Hamas waliwaua watu 1,200 hivi na kuchukua mateka zaidi ya watu 200.
Watu wakitembea kuvipita vifusi vya majengo yaliyobomolewa katika operesheni ya kijeshi ya Israel kwenye eneo la Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 17, 2023. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma