Lugha Nyingine
Watu 32 wauawa kwenye mapigano makali ya kikabila katika mkoa wa Abyei karibu na Sudan Kusini
Watu 32 wameuawa kwenye mapigano makali ya kikabila yaliyotokea katika Jimbo la Abyei lililoko katika mpaka wa Sudan Kusini na Sudan jana Jumapili.
Akizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua, Katibu Mkuu wa Serikali ya Jimbo la Abyei, Arou Manyiel Arou amesema, mapigano hayo yalitokea mapema siku hiyo kufuatia shambulio la kulipiza kisasi kwa kabila la Ngok Dinka katika maeneo ya Wuncuei na Nyiel jimboni humo lililofanywa na vijana waliokuwa na silaha kutoka Kaunti ya Twic ya jimbo jirani la Warrap, nchini Sudan Kusini.
Amesema shambulio la karibuni la kulipiza kisasi limetokea baada ya mapigano ya wiki iliyopita katika eneo la Ayuok kati ya pande hizo mbili, na kusababisha vifo vya watu 34, akiwemo askari wa Jeshi la Sudan Kusini. Ameongeza kuwa, pande hizo mbili zimekuwa na mvutano wa muda mrefu kugombea eneo la ardhi katika eneo la mpakani la Aneet, ambalo linatenganisha makabila hayo mawili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma