Spika wa Bunge la Umma la China afanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Duma la Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 22, 2023

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Duma la Russia, Vyacheslav Volodin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Novemba 21, 2023. (Xinhua/Pang Xinglei)

Beijing – Spika wa Bunge la Umma la China Zhao Leji amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Duma la Russia, Vyacheslav Volodin siku ya Jumanne mjini Beijing, akitoa wito wa kuimarishwa kwa mabadilishano kati ya mabunge ya nchi hizo mbili.

Kwenye mkutano huo Zhao amesema, chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na uratibu katika zama mpya kati ya China na Russia umedumisha mwelekeo sahihi wa kimaendeleo. Kuaminiana kisiasa kumeimarishwa kila mara, ushirikiano wa kivitendo umefanywa kwa nguvu na mabadilishano kati ya watu na ya serikali za mitaa yameendelea kuimarishwa, na kuweka mfano wa kuigwa wa mtindo mpya wa uhusiano kati ya nchi kubwa.

Zhao amesema, haijalishi hali ya kimataifa itabadilika vipi, China na Russia zinapaswa kushirikiana ili kuunganisha na kuendeleza uratibu wa kimkakati wa pande zote, kuleta manufaa kwa watu wa pande hizo mbili, na kulinda haki na usawa wa kimataifa.

Amesema pande hizo mbili zinapaswa kuendelea kuhimiza muunganisho kati ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia, kufikia manufaa zaidi ya ushirikiano wa kivitendo, na kuhamasisha ushirikiano katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO, BRICS na mifumo mingine.

Zhao amesema kamati ya ushirikiano wa kibunge kati ya China na Russia ni jukwaa thabiti na lenye ufanisi kwa ajili ya kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuhimiza ushirikiano wa kivitendo na kuendeleza urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Volodin amesema kuwa Russia inashikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kwamba pande na vikundi vyote vya Bunge la Duma la Russia vinaunga mkono maendeleo endelevu ya uhusiano wa kirafiki na China.

Amesema, Bunge la Duma la Russia, liko tayari kufanya juhudi za pamoja na Bunge la Umma la China ili kutekeleza jukumu chanya la kamati ya ushirikiano wa kibunge kati ya Russia na China, kutoa hakikisho la kisheria la kuendeleza ushirikiano wa kivitendo baina ya nchi hizo mbili, na kuchangia katika maendeleo ya uhusiano kati ya Russia na China. 

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Duma la Russia, Vyacheslav Volodin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Novemba 21, 2023. (Xinhua/Pang Xinglei)

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Duma la Russia, Vyacheslav Volodin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Novemba 21, 2023. (Xinhua/Pang Xinglei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha