

Lugha Nyingine
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapitisha azimio kuhusu Usimamishaji vita wakati wa Michezo ya Olimpiki
Picha iliyopigwa Septemba 14, 2020 ikionyesha mandhari ya nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. (Xinhua/Wang Ying)
UMOJA WA MATAIFA - Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kuhusu Kusimamisha Vita wakati wa Michezo ya Olimpiki siku ya Jumanne ambalo linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuzingatia azimio hilo mmoja mmoja na kwa pamoja katika kipindi kizima cha kuanzia siku ya saba kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris hadi siku ya saba baada ya kumalizika kwa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Paris Mwaka 2024.
Rasimu ya azimio hilo imeletwa kwa ajili ya kupigiwa kura kwa ombi la Russia. Azimio hilo limepitishwa kwa kura 118 za Ndiyo na hakuna kura ya Hapana huku nchi wanachama wawili wakiwa hawakupiga kura. Russia na Syria hazikupiga kura.
Kabla ya upigaji kura, Naibu Balozi wa Kudumu wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa Maria Zabolotskaya alisema wawezeshaji wa Ufaransa wa rasimu hiyo "walifuata njia ya kundi la nchi za Magharibi" na kuwasilisha rasimu ya azimio lisilo na "kanuni za sawa, kuondoka siasa kwenye michezo au kupinga ubaguzi."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma