

Lugha Nyingine
Bunge la Afrika Kusini lapitisha muswada wa kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel
(CRI Online) Novemba 22, 2023
Bunge la Afrika Kusini limepitisha muswada wa kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel siku ya Jumanne kufuatia matokeo ya kura zilizopigwa na wabunge, ambapo kura 248 ziliunga mkono muswada huo na kura 91 ziliupinga.
Baada ya kupitisha muswada huo, Bunge hilo lilisema, muswada huo hauingilii serikali kisheria, lakini Spika ana jukumu la kuwasilisha muswada huo kwa rais na idara husika za serikali.
Hata hivyo, Jumatatu wiki hii, Baraza la Mawaziri la Afrika Kusini lilitangaza kuwa bado halijaamua iwapo litafunga Ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma