

Lugha Nyingine
Wilaya ya Bortala katika Mkoa wa Xinjiang, China: Bandari yenye nguvu ya nchi kavu inayoharakisha ufanisi wa viwanda
Bortala inamaana “mbuga ya kijani” katika lugha ya Kimongolia. Mandhari ya mazingira asilia katika Wilaya hii iliyoko Mkoa wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China ni yenye kuvutia. Maziwa makubwa, mbuga za kijani, ardhi oevu yenye mimea iliyostawi hukuza wakazi wataratibu na wema huko.
Wilaya hii ambayo ni kituo muhimu cha zamani cha usafiri kando ya “Njia ya Kale ya Hariri” sasa inasimama kama mstari wa mbele wa sera ya China ya kufungua mlango kwa nchi za Magharibi, na imeendelea hadi kuwa stesheni muhimu ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje wa China katika “Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri”. Wilaya ya Bortala inatumia kikamilifu njia hii muhimu ya biashara kati ya China na Ulaya kuiwezesha zaidi China kuchangia na Dunia manufaa ya maendeleo yake ya ufungaji mlango wa kiwango cha juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma