Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya Biashara ya Kidigitali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2023

Beijing - Rais wa China Xi Jinping ametuma barua ya pongezi kwa Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya Biashara ya Kidijitali, ambayo yanafanyika kuanzia Novemba 23 hadi 27 huko Hangzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, akisema kuwa kushamiri kwa biashara ya kidijitali duniani kumefuatiliwa zaidi na kutakuwa ongezeko jipya katika biashara ya kimataifa.

Amesema, katika miaka ya hivi karibuni, China imefanya jitihada za kuendana kikamilifu na kanuni za uchumi na biashara za kimataifa zenye vipimo vya juu, kuanzisha na kuboresha mifumo yake ya udhibiti wa biashara ya kidijitali, na kuhimiza mageuzi na uvumbuzi wa biashara ya kidijitali.

“Kwa kufanya hivyo, China imekuwa ikitoa fursa mpya kwa dunia kupitia maendeleo yake mapya,” Rais Xi amesema.

Ametoa wito wa kutumia kikamilifu maonyesho hayo ili kuongeza ushirikiano, kutafuta maendeleo kwa pamoja na kuchangia manufaa, kujenga biashara ya kidijitali kuwa injini mpya ya maendeleo ya pamoja, na kutia msukumo mpya katika ukuaji wa uchumi wa Dunia.

Yakiwa na kaulimbiu isemayo "Biashara ya Kidijitali Yashamiri Duniani," maonyesho hayo yameandaliwa kwa pamoja na serikali ya Mkoa wa Zhejiang na Wizara ya Biashara ya China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha