

Lugha Nyingine
China yaitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi ili kuhimiza suluhu ya Nchi Mbili katika suala la Palestina
Mjumbe wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi ili kuhimiza mchakato wa kisiasa wa kufanya upya suluhu ya kuunda Nchi Mbili katika kusuluhisha mgogoro kati ya Israel na Palestina.
Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel Balozi Zhang amesema, mpango wowote wa utatuzi wa hali ya sasa hauwezi kuachana na suluhu ya Nchi Mbili, na lazima usaidie amani na utulivu wa kikanda.
Amesema mpango wowote unaohusisha hatma ya Palestina lazima ukubaliwe na Wapalestina, na kuzingatia masuala yanayogusa haki za nchi za kikanda.
Balozi Zhang pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi ili kufikia usimamishaji mapigano mara moja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma