

Lugha Nyingine
China yachukua hatua kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya katika mfumo wa kupumua
BEIJING - China inachukua hatua kushughulikia ongezeko la hivi majuzi la maambukizi ya katika mfumo ya kupumua yanayosababishwa na vimelea tofauti vya kupumua wakati nchi hiyo inaingia majira ya baridi, Mi Feng, Msemaji wa Kamati Taifa ya Afya ya China, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili huku akisema katika siku za hivi karibuni magonjwa ya kupumua ya kuambukiza hasa yametokana na virusi vya mafua, na visa vingine vinavyosababishwa na virusi vya rhino, nimonia ya mycoplasma, virusi vya upumuaji vya syncytial, na virusi vya adeno.
Amesema, kamati hiyo imeagiza serikali za mitaa kuhakikisha utekelezaji wa upimaji na utoaji wa matibabu ulioainishwa na kutoa taarifa kwa umma kuhusu vituo vya tiba vyenye huduma za watoto na kliniki za homa ili kusaidia wagonjwa kupata hospitali iliyo karibu nao.
“Juhudi zinapaswa kufanywa ili kuongeza vyumba vya ushauri na maeneo ya matibabu ya magonjwa hayo, kuongeza ipasavyo muda wa utoaji wa huduma, kuhakikisha ugavi wa dawa, na kutumia kikamilifu jukumu la dawa za kijadi za China, Mi amesema, huku akisisitiza umuhimu wa kukabiliana na maambukizi katika shule, chekechea, nyumba za wazee, na sehemu nyingine muhimu zilizo na idadi kubwa ya watu.
China pia imehimiza matibabu ya mtandaoni ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa, kutumia kikamilifu majukwaa mtandaoni ya hospitali ili kuweka mazingira wezeshi ya kliniki za homa na matibabu ya watoto.
“Chanjo inaendelea kuwa hatua yenye ufanisi zaidi ya kukinga maambukizi kwa wazee, hasa wale walio na magonjwa mengine sugu, amesema Li Yanming, mkuu wa idara ya dawa tiba za upumuaji na huduma za dharura katika Hospitali ya Beijing.
Li amesisitiza umuhimu wa kudumisha halijoto na unyevunyevu ufaao katika mazingira ya nyumbani.
Amesema mazingira makavu ya kupita kiasi nyumbani pia hayafai kwa afya ya mfumo wa kupumua. Amewakumbusha wazee waepuke sehemu zenye watu wengi na za ndani na kuwashauri kuvaa barakoa wanapokuwa nje.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma