

Lugha Nyingine
China, Japan na Korea Kusini zinapaswa kutoa mchango mkubwa zaidi wa kivitendo katika kuhimiza maendeleo ya kikanda na kimataifa: Wang Yi
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akihudhuria mkutano wa kumi wa mawaziri wa mambo ya nje wa pande tatu za China, Japan na Korea Kusini pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Park Jin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Yoko Kamikawa mjini Busan, Korea Kusini, Novemba 26, 2023. (Xinhua/Yao Qilin)
BUSAN, Korea Kusini - China, Japan na Korea Kusini zinapaswa kutoa mchango mkubwa zaidi wa kivitendo katika kuhimiza maendeleo ya kikanda na kimataifa yanayokabiliwa na mabadiliko ya kasi ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita na kuimarika taratibu kwa uchumi wa Dunia, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema Jumapili alipohudhuria mkutano wa 10 wa mawaziri wa mambo ya nje wa pande tatu za China, Japan na Korea Kusini pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Park Jin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Yoko Kamikawa mjini Busan, Korea Kusini.
Wang, mbaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema kuwa ushirikiano kati ya China na Japan na Korea Kusini umekuwa mfumo kazi wa ushirikiano wa pande nyingi wenye kiwango cha juu zaidi cha utaratibu , unaohusisha maeneo mapana na mambo mengi zaidi katika Asia ya Mashariki ambayo imesaidia vyema maendeleo ya nchi hizo tatu na kunufaisha watu wa eneo hilo.
“Kufuatia sera ya kujenga urafiki na ushirikiano na majirani zake, China itaendelea kushirikiana na Korea Kusini na Japan kurudisha ushirikiano wa pande tatu kwenye njia ya kawaida, kudumisha hali nzuri ya utulivu na maendeleo endelevu, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya amani na ustawi wa kikanda na Dunia” amesema Wang.
Amesisitiza kuwa, kipaumbele cha juu ni kuendelea kuheshimu njia ya maendeleo ya kila mmoja na masilahi ya msingi, kushughulikia ipasavyo masuala nyeti na kudumisha uhusiano mzuri wa pande mbili, ili kuweka msingi imara kwa kuanzisha tena ushirikiano wa pande tatu ili kutimiza maendeleo ya muda mrefu kwa hatua madhubuti.
Wang amesisitiza kuwa nchi hizo tatu zinapaswa kushikilia ushirikiano wa kunufaishana na kupata matokeo yenye manufaa kwa pande zote, kuanzisha upya majadiliano ya makubaliano ya biashara huria ya pande tatu za China, Japan na Korea Kusini haraka iwezekanavyo, kudumisha kasi ya mafungamano ya kiuchumi ya kikanda, kuboresha njia mbalimbali na mipango ya ngazi mbalimbali ya biashara huria ya kikanda, ili kuchangia katika lengo la pamoja la kusukuma uanzishaji wa Eneo la Biashara Huria la Asia-Pasifiki.
Kwa upande wao Park na Kamikawa wamepongeza hatua iliyofikiwa katika ushirikiano wa China, Japan na Korea Kusini, wakisema kuwa nchi hizo tatu ni majirani wasioweza kutenganishwa na ushirikiano wa pande tatu una umuhimu mkubwa na uwezo mkubwa wa kifursa.
Pembezoni mwa mkutano huo, Wang pia alifanya mikutano ya pande mbili na Park na Kamikawa mtawalia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akihudhuria mkutano wa kumi wa mawaziri wa mambo ya nje wa pande tatu za China, Japan na Korea Kusini pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Park Jin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Yoko Kamikawa mjini Busan, Korea Kusini, Novemba 26, 2023. (Xinhua/Yao Qilin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma