Xi Jinping aongoza mkutano wa viongozi kuhusu maendeleo ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang na uongozi wa CPC kuhusu mambo ya nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 28, 2023

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano siku ya Jumatatu ulioongozwa na Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC ili kupitia “Maoni kuhusu sera na hatua za kuhimiza zaidi maendeleo yenye ubora wa juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang” na “Kanuni za uongozi wa CPC juu ya mambo ya nje".

Mkutano huo umebainisha kuwa mkakati wa kuendeleza Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang ni uamuzi mkubwa wa kimkakati uliofanywa na Kamati Kuu ya CPC na kwamba kuendeleza maendeleo yenye ubora wa juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang kunategemea kimsingi ikolojia nzuri ya maeneo ya mtiririko wa Mto Changjiang .

Umesisitiza juhudi katika ulinzi wa hali ya juu wa maeneo ya mtiririko wa Mto Changjiang, na mstari mwekundu wa kiikolojia ambao umechorwa lazima uimarishwe na kuwekwa chini ya uangalizi.

Mkutano huo umeeleza kuwa, ni lazima kufanya uratibu na juhudi za pamoja katika kuhimiza kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kuongeza uoto wa mimea na kuendeleza ukuaji wa kiuchumi.

Mkutano huo umesisitiza jukumu la uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia katika kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang, na kuagiza kufanya juhudi za kuratibu mpangilio na uhamishaji wa viwanda kando ya Mto Changjiang.

Mkutano huo umesisitiza haja ya kuimarisha zaidi uongozi wa juu wa Kamati Kuu ya CPC kuhusu mambo ya nje, na kuharakisha juhudi za kuunda mfumo kamili wa sheria na kanuni kuhusu masuala yanayohusiana na mambo ya nje.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha