

Lugha Nyingine
China inakaribisha juhudi zote muafaka kwa kusimamisha vita na kutuliza hali ya Gaza: Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje
(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.)
China inakaribisha juhudi zote ambazo ni muafaka kwa ajili ya kuleta usimamishaji vita na kutuliza hali, amesema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin alipozungumzia suala la Palestina na Israel siki ya Jumatatu.
Wang amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari wa mara kwa mara alipoulizwa kutoa maoni juu ya hali ya sasa ya Gaza.
“Ni hatua kuelekea amani, hata hivyo ni ndogo, inapaswa kuhamasishwa. Changamoto katika kulinda raia, hata hivyo changamoto ya kutisha inapaswa kushindwa kwa kila juhudi iwezekanavyo,” amesema Wang.
Huku akisisitiza duru ya sasa ya mgogoro kati ya Palestina na Israel imeendelea kwa zaidi ya siku 50 na kusababisha vifo na majeruhi ya watu wengi na majanga ya kibinadamu, Wang amesema vurugu hazileti usalama wa kweli na matumzi ya nguvu za kijeshi hayataweza kuleta amani ya kudumu.
China inakaribisha juhudi zote ambazo ni muafaka katika kuleta usimamishaji vita na kutuliza hali, amesema Wang, huku akitaka pande husika katika mgogoro huo kutekeleza vizuri Azimio Namba 2712 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na azimio lililopitishwa na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake maalumu wa dharura, kutekeleza kwa pamoja na ipasavyo makubaliano ya sasa ya kusimamisha vita kwa muda na kuyawezesha kuongezwa muda, na kufikia kusitisha vita kwa kweli na kwa kudumu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma