

Lugha Nyingine
China kuimarisha uhusiano na kuongeza ushirikiano na Kazakhstan: Naibu Waziri Mkuu wa China
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev mjini Astana, Kazakhstan, Novemba 27, 2023. (Xinhua/Yan Yan)
ASTANA - China iko tayari kushirikiana na Kazakhstan kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuhimiza ujenzi wa kiwango cha juu wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), na kusukuma ushirikiano wa kudumu wa kimkakati kati ya China na Kazakhstan katika ngazi ya juu, amesema Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang siku ya Jumatatu, alipokutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev mjini Astana wakati wa ziara yake nchini humo Novemba 26 na 27.
Ding ambaye pia mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amewasilisha salamu za dhati na za kutakia kheri za Rais wa China Xi Jinping kwa Tokayev.
Akieleza kuwa ushirikiano kati ya China na Kazakhstan una msingi imara, uwezo mkubwa na matarajio mapana ya kifursa, Ding amesema China iko tayari kushirikiana na Kazakhstan ili kuimarisha msingi wa kuaminiana, kuimarisha muunganisho wa mikakati ya maendeleo, kuimarisha uratibu wa sera na kupanua ushirikiano wa kunufaishana ili kusaidiana kufikia malengo yao ya maendeleo.
Ding ametoa wito kwa pande hizo mbili kuongeza muunganisho kati ya BRI na Pendekezo la Njia ya Mustakabali Mzuri la Kazakhstan, kutafuta kikamilifu aina mpya na njia za ushirikiano, na kuimarisha ushirikiano katika utamaduni, utalii, elimu, michezo, vijana na katika serikali za mitaa ili kuendelea mbele urafiki wa jadi kati ya China na Kazakhstan.
Ameongeza kuwa China iko tayari kushirikiana na Kazakhstan kuhimiza ufanisi thabiti wa mifumo ya China na Asia ya Kati ili kudumisha kwa pamoja amani na utulivu wa kikanda.
Kwa upande wake Tokayev amemuomba Ding kufikisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi wa China, na kusema kuwa Kazakhstan inaunga mkono kithabiti ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na inakaribisha kampuni za China kuwekeza nchini Kazakhstan.
Katika ziara yake hiyo nchini Kazakhstan, Ding pia alikutana na Waziri Mkuu wa Kazakhstan Alikhan Smailov, na Ding na Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Kazakhstan, Roman Sklyar waliendesha pamoja Mkutano wa 11 wa Kamati ya Ushirikiano ya China na Kazakhstan.
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev mjini Astana, Kazakhstan, Novemba 27, 2023. (Xinhua/Yan Yan)
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri Mkuu wa Kazakhstan Alikhan Smailov mjini Astana, Kazakhstan, Novemba 27, 2023. (Xinhua/Li Tao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma