

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuongoza mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la UN kuhusu suala la Palestina na Israel
Beijing – China ikiwa Mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa Mwezi Novemba, itafanya mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel Novemba 29. ambapo Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi atakwenda New York kuongoza mkutano huo.
Habari ya mkutano huo wa ngazi ya juu imetolewa na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin siku ya Jumatatu.
Duru hii ya mgogoro kati ya Palestina na Israel imesababisha vifo vingi vya raia na maafa ya kibinadamu, na jumuiya ya kimataifa imefuatilia sana hali hiyo . China inatarajia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutekeleza jukumu lake la msingi la kudumisha amani na usalama wa kimataifa, na kufanya kazi yake ya kiujenzi, msemaji Wang amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari wa kila siku.
Amesema, Azimio nambari 2712, ambalo ni azimio la kwanza kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya duru ya sasa ya mgogoro wa Palestina na Israel kuzuka na pia ni la kwanza kupitishwa kuhusu suala la Palestina na Israel tangu mwisho wa Mwaka 2016, limehimiza hatua za awali za usimamishaji wa mapigano na ni muafaka katika kuepuka msukosuko wa ubinadamu na balaa.
“China inatumai kuwa kwa kufanya mkutano huo wa ngazi ya juu, pande zote zinaweza kuhimiza mazungumzo ya kina na kujenga maelewano, kuchukua hatua madhubuti na kutoa mchango unaostahili kwa ajili ya kupunguza msukosuko wa ubinadamu huko Gaza, kufikia usimamishaji vita na usitishaji wa mapigano, kulinda raia na hatimaye kuhimiza utatuzi wa suala la Palestina kwa pande zote kwa haki na kudumu,” amesema msemaji huyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma