Mchana mfanya kazi ofisini, lakini jioni mwanafunzi – mtindo mpya wa maisha ya vijana wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 29, 2023

Watu wakihudhuria darasa la kaligrafia katika Kituo cha Ushirikiano kilichoko eneo la Jiangbei katika Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China Novemba 24, 2023. (Picha na Wang Chao/Xinhua)

Watu wakihudhuria darasa la kaligrafia katika Kituo cha Ushirikiano kilichoko eneo la Jiangbei katika Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China Novemba 24, 2023. (Picha na Wang Chao/Xinhua)

Kote China, vijana wengi wanaofanya kazi za kuajiriwa maofisini wanachagua kwenda shule ya usiku. Hapo zamani madarasa ya jioni yaliweka mkazo zaidi kwenye maendeleo ya kitaaluma au utaalam, lakini sasa, hata hivyo, kozi mbalimbali, kuanzia uigizaji hadi sanaa ya ukataji karatasi, zimejitokeza, ambazo siyo tu zinaburudisha bali pia kubadilisha mtindo wa maisha ya wakazi mijini.

Liu Shuang, Mchezesha Disko (DJ) mwenye umri wa miaka 25, ni mwendaji wa mara kwa mara kwenye Mtaa wa Tisa wa Mji wa Chongqing, China, lakini badala ya kuelekea kwenye bar, uelekeo wake ni katika kituo cha utamaduni, ambako anafundisha darasa la u-DJ.

“Hapo zamani DJ angeleta sanduku zito la kubeba sahani za santuri kwenye maonesho,” Liu alifafanua kwenye darasa lake lenye wanafunzi zaidi ya 20. Kozi anayofundisha Liu ni moja kati ya madarasa mengi yanayowezeshwa na kituo hicho tangu kilipoanza kutoa madarasa ya jioni mwezi wa Agosti.

Wakati darasa lilipoingia kipindi cha masomo kwa vitendo, Zhou Mozi mwenye umri wa miaka 61 alinyoosha mkono wake haraka kati ya kundi la wanafunzi ambao wengi wao ni vijana, na kuruka jukwaani.

“Inavutia sana, na nitakuja tena. Ninataka kuungana na vijana,” amesema Zhou, huku akieleza kuwa aliona picha ya bango la kozi hiyo iliyotumwa na mhudumu wa mtaa wa eneo lake kwenye Kundi la Wechat (program ya mawasiliano ya China) na kujisajili mara moja.

Tangu kilipoanza kutoa madarasa ya jioni, Kituo cha Ushirikiano, ambacho ni eneo maalum la utamaduni na ubunifu katika eneo la Jiangbei, kimekuwa na pilikapilika za shughuli mbalimbali, kikiwa na wanafunzi zaidi ya 900 wanaohudhuria madarasa ya uigizaji, uonyeshaji mitindo, kaligrafia, uandaaji wa kahawa na ujuzi wa kuchanganya vinywaji mbalimbali (cocktail).

Katika miezi miwili iliyopita, wakazi zaidi ya 1,000 wa Chongqing wameshiriki kwenye aina tofauti za madarasa ya jioni.

Licha ya Chongqing, Shanghai, Chengdu na majiji mengine ya China pia yamezindua madarasa mbalimbali ya jioni, ambayo yanapendwa sana. Kwa mujibu wa takwimu kutoka majukwaa ya mtandaoni ya China, Meituan na Dianping, idadi ya watu wanaotafuta mtandaoni neno “shule ya usiku” imeongezeka kwa asilimia 980 kuliko kipindi hicho mwaka uliopita.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha