Mji wa Shenzhen, China: Kituo kinachokua kwa kasi cha uanamitindo na mitindo ya urembo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2023

Shenzhen, ni mji mpya zaidi wa daraja la kwanza nchini China, mara nyingi huhusishwa na teknolojia, uvumbuzi, na kasi. Hata hivyo, utamaduni motomoto wa mitindo ya urembo unaibuka kwa kasi na kuingiliana na sifa za ukuaji na umaalum wa kitamaduni wa mji huu, na kuunda mtindo wa kipekee.

"Chapa za Shenzhen" na "Miundo ya Shenzhen" inajitokeza pamoja na maendeleo ya mji. Tasnia ya saa ni sehemu muhimu ya sekta ya mitindo ya kisasa ya Shenzhen. Mji huo ni nyumbani kwa kampuni 1,500 za saa, zikizalisha thamani ya mapato ya kila mwaka ya yuan bilioni 68. Uzalishaji wa saa wa Shenzhen unachukua asilimia 53 ya uzalishaji wote wa China na asilimia 42 ya uzalishaji wote duniani. Time Valley, kitovu cha tasnia ya saa mjini Shenzhen na China, ni makao ya kampuni 6 kati ya 10 bora za saa za China.

Ukiacha saa za mkononi na ukutani, vito vya dhahabu ni alama nyingine ya tasnia ya mitindo ya Shenzhen. Eneo la Kibiashara la Vito vya Dhahabu la Shuibei, ambalo ni kituo kikubwa zaidi na cha juu zaidi cha vito vya dhahabu nchini China chenye mnyororo mpana wa kiviwanda, kinajivunia mapato ya uendeshaji ya kila mwaka yanayozidi yuan bilioni 100. Hii inawakilisha asilimia takriban 50 ya sehemu ya soko la China katika uuzaji wa jumla wa vito vya dhahabu.

Mitaa ya Shenzhen ni maonyesho ya mitindo. Ikiwa umevaa vizuri au katika mavazi rahisi, katika mji huu jumuishi na wenye kupendeza, "kuwa mwenyewe" ni maana halisi ya mwisho ya mtindo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha