Mafunzo ya uboreshaji aina za nazi na kukinga Magonjwa na Wadudu Waharibifu wa Mimea yakamilika Zanzibar, Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2023

Hafla ya mahafali ya mafunzo ya kozi ya uboreshaji wa aina za nazi na kukinga magonjwa na wadudu waharibifu wa mimea visiwani Zanzibar, Tanzania imefanyika kwenye Chuo cha Utalii cha Chuo Kikuu cha Zanzibar tarehe 28 mweizi huu.

Mafunzo ya kozi hiyo ya siku 50 yamefadhiliwa na Wizara ya Biashara ya China, na kuendeshwa na Taasisi Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Kilimo cha Kitropiki ya China. Taasisi hiyo iliandaa wataalamu sita wa nyanja za nazi na kinga dhidi ya magonjwa na wadudu waharibifu kufundisha darasa la mafunzo hayo, ambayo yalihusisha ukuzaji, upandaji na ukingaji wa miche ya minazi dhidi ya wadudu waharibifu, na teknolojia ya kudhibiti wadudu hao waharibifu kwa miembe, migomba, mboga, mihogo na mimea ya mazao mbalimbali.

Wapokeaji wa mafunzo hayo wamesema, mafunzo yalihusisha maudhui na vitendo halisi vingi, na wamepata ujuzi mwingi. Wamesema, siku za baadaye watafundisha ujuzi huo kwa wakulima, ili kwamba matunda ya mafunzo hayo yaweze kunufaisha watu wengi zaidi.

Katika hatua inayofuata, pande hizo mbili za China na Tanzania zitaendelea kufanya ushirikiano wa nguvu kazi, na kutumia mafunzo ya kozi hizo kama fursa ya kuimarisha ushirikiano katika sayansi na teknolojia ya kilimo cha kitropiki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha