Kampuni ya China zasaini makubaliano ya kuongeza usambazaji wa bidhaa za mtandao wa intaneti kwa Afrika Mashariki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2023

Kampuni ya FiberHome International Technologies ya China imetia saini makubaliano na kampuni ya CP Cables ya Kenya ili kuongeza usambazaji wa bidhaa za mtandao wa intaneti yenye kasi katika soko la Afrika Mashariki.

Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa FiberHome International Technologies Bw. Bruce Wang, amewaambia wanahabari mjini Nairobi kwamba kutokana na makubaliano hayo ya miaka miwili, kampuni ya CP Cables itakuwa msambazaji mkuu wa bidhaa zao nchini Kenya na Uganda.

Makubaliano hayo yatawezesha Afrika Mashariki kupata bidhaa za hali ya juu zitakazosaidia watumiaji kunufaika na intaneti ya kasi kwa bei nafuu.

Bw. Wang amesema kampuni ya FiberHome imejitolea kuunga mkono lengo la Kenya la kuweka mtandao wa mkongo wa intaneti kote nchini ili kupanua ufikiaji wa mtandao wa intaneti wa njia pana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha