

Lugha Nyingine
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC ahitimisha uchunguzi wa ghasia za uchaguzi wa 2007 nchini Kenya
Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Nazhat Shameen Khan ametangaza Jumatatu kwamba anafuta uchunguzi zaidi kuhusu uhalifu uliofanyika nchini Kenya kuhusiana na ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Uamuzi huo unahitimisha sakata hilo la kisheria lililoendelea kwa miaka 13 ambalo liliwahusisha wanasiasa wakuu wa Kenya. Kwenye taarifa yake Nazhat Shameen Khan amesema amefikia uamuzi huu baada ya kuzingatia ukweli maalum na mazingira ya halisia.
Sambamba na hilo, amesema ofisi yake haitafuatilia kesi za ziada katika madai ya jinai ya watu wengine.
Mwaka 2010, mahakama hiyo yenye makao yake mjini The Hague ilianza kuchunguza mapigano baada ya uchaguzi katika taifa hilo ambapo waendesha mashtaka walisema watu 1,300 walikufa na wengine 600,000 waliachwa bila makazi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma