Kampuni ya China yatoa vitabu zaidi ya 500 kwa chuo kikuu cha Misri

(CRI Online) Novemba 30, 2023

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Kampuni ya mafuta ya petroli ya China Sinopec imetoa vitabu zaidi ya 500 kwa Chuo Kikuu cha China cha Misri (ECU), vyenye maudhui mchanganyiko ya lugha za Kichina, Kiarabu, Kichina-Kiarabu, na Kichina-Kiingereza, vikihusu mambo ya dawa za kijadi za Kichina, utamaduni wa Kichina, fedha, uchumi, usimamizi, biashara ya mtandaoni na ufundishaji wa lugha ya Kichina.

Akiongea mjini Cairo kwenye hafla ya kukabidhi vitabu hivyo, ofisa mwandamizi wa ubalozi wa China nchini Misri Lu Chunsheng, amesema huu ni mwaka wa kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja”(BRl), na China na Misri ni washirika wa jadi katika ujenzi wa ukanda huo.

Bwana Lu amesema vitabu hivyo vitawapa walimu na wanafunzi mtazamo mpya wa kuthamini utajiri wa historia, utamaduni na lugha ya Kichina, na kupata ufahamu kuhusu maendeleo ya jamii ya kisasa ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha