Rais Xi Jinping asisitiza kupata mafanikio mapya makubwa katika maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Changjiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 01, 2023

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiongoza kongamano la kusukuma mbele maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Changjiang na kutoa hotuba muhimu mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 30, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

SHANGHAI - Rais wa China Xi Jinping siku ya Alhamisi alipokuwa akiongoza kongamano la kuendeleza maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Changjiang, amesisitiza kufanya juhudi za kupata mafanikio mapya makubwa katika maendeleo jumuishi ya delta hiyo na kuimarisha mchango wake wenye mfano wa kuigwa katika kujenga mambo ya kisasa ya China.

Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesisitiza umuhimu wa kuendeleza maendeleo jumuishi ya eneo hilo, kuboresha uwezo wake wa uvumbuzi, ushindani wa kiviwanda na ubora wa maendeleo, na kujenga muundo mpya wa mageuzi na kufungua mlango kwa kiwango cha juu.

"Haya ni muhimu sana kwa China kujenga dhana mpya ya maendeleo, kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu, na kuendeleza ujenzi wa nchi yenye nguvu na ustawishaji wa taifa kupitia njia ya China kuelekea maendeleo ya mambo ya kisasa," amesema.

Amesisitiza kwamba ni muhimu kutekeleza kikamilifu na kwa usahihi dhana mpya ya maendeleo katika sekta zote, kujikita katika ujumuishi na ubora wa juu, kuwa na maono ya dunia nzima na kufikiri kimkakati, kuendeleza kwa kina mageuzi na kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu bila kulegalega, na kuratibu uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia pamoja na uvumbuzi wa viwanda, kuratibu muunganisho wa vifaa na mashine na ushirikiano wa kimfumo, na kuratibu kazi ya ulinzi wa mazingira na maendeleo ya kiuchumi, ili kupata mafanikio mapya makubwa katika maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Changjiang.

“Nguvu ya jumla ya kifursa na ushindani wa pande zote wa Delta ya Mto Changjiang unaendelea kushika nafasi ya juu nchini,” amesema Rais Xi.

Kuhusu maendeleo ya siku zijazo, Rais Xi amesisitiza kuimarisha ushirikiano wa kuvuka eneo zima hilo la delta katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia na uvumbuzi wa kiviwanda.

Amesema juhudi zinapaswa kufanywa ili kuzalisha viwanda vipya, miundo na mitindo mipya ya biashara, na kuongeza nafasi mpya ya maendeleo.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang, pamoja na mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama Cai Qi na maofisa viongozi wengine walihudhuria kongamano hilo.

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiongoza kongamano la kusukuma mbele maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Changjiang na kutoa hotuba muhimu mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 30, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiongoza kongamano la kusukuma mbele maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Changjiang na kutoa hotuba muhimu mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 30, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha