Wizara ya Mambo ya Nje ya China yatoa waraka wa msimamo wa China juu ya utatuzi wa mgogoro kati ya Palestina na Israel

(CRI Online) Desemba 01, 2023

Wizara ya Mambo ya Nje ya China siku ya Alhamisi, Novemba 30 imetoa waraka kuhusu msimamo wa China juu ya utatuzi wa mgogoro kati ya Palestina na Israel.

Waraka huo unasema mgogoro huo umesababisha vifo na majeruhi ya raia wengi, pamoja na janga la kibinadamu, ambapo jumuiya ya kimataifa inafuatilia zaidi mgogoro huo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa, China inatoa mapendekezo yafuatayo: Kwanza, pande zote kusitisha vita. Pili, kuwalinda raia ipasavyo. Tatu, kuhakikisha msaada wa kibinadamu. Nne, kuimarisha usuluhishi wa kidiplomasia. Tano, kutafuta suluhu ya kisiasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha